Daniel 4:22 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, ni wewe ee mfalme ambaye umekuwa mkubwa na mwenye nguvu. Ukuu wako umefika mpaka mbinguni, na ufalme wako umeenea mpaka miisho ya dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu; nao ukuu wako umekua hadi kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea hadi miisho ya dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, ni wewe ee mfalme ambaye umekuwa mkubwa na mwenye nguvu. Ukuu wako umefika mpaka mbinguni, na ufalme wako umeenea mpaka miisho ya dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu, ukuu wako umekua mpaka kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea mpaka miisho ya dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu, nao ukuu wako umekua mpaka kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea mpaka miisho ya dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe mfalme ndiwe mti huo, kwani u mkuu mwenye nguvu, ukuu wako umekua, ukafika hata mbinguni, ukatawala mpaka kwenye mapeo ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe utafukuzwa mbali na wanadamu. Utaishi pamoja na nyama wa pori, utakula majani kama ngombe; utalowana na umande wa mbinguni. Utakaa katika hali hiyo kwa miaka saba, na kwa mwisho utatambua kwamba Mungu Mukubwa ndiye anayetawala juu ya ufalme wa wanadamu naye anamupa ufalme ule mutu yeyote anayemutaka.