Daniel 4:26 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena amri ile ya kukiacha kisiki na mizizi ya mti huo ardhini ina maana hii: Wewe utarudishiwa tena ufalme wako hapo utakapotambua kwamba Mungu wa mbinguni ndiye atawalaye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejeshwa kwako utakapokubali kwamba Mbingu ndizo hutawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena amri ile ya kukiacha kisiki na mizizi ya mti huo ardhini ina maana hii: Wewe utarudishiwa tena ufalme wako hapo utakapotambua kwamba Mungu wa mbinguni ndiye atawalaye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejezwa kwako utakapokubali kwamba Mbingu ndizo zitawalazo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejezwa kwako utakapokubali kwamba Mbingu ndizo zitawalazo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo wakisema, waliache shina lenye mizizi yake huo mti, ni kwamba: Ufalme wako utakurudia tena hapo, utakapojua, ya kuwa mbingu ndizo zitawalazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya miezi kumi na miwili, mufalme Nebukadneza alikuwa anatembea juu ya dari ya nyumba ya kifalme katika muji wa Babeli.