Daniel 4:27 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo, ee mfalme, sikiliza shauri langu. Achana na dhambi zako na maovu yako, utende haki na kuwaonea huruma waliodhulumiwa; huenda muda wako wa fanaka ukarefushwa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, ee mfalme, uwe radhi kupokea ushauri wangu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako na uwe na huruma kwa waliodhulumiwa. Hivyo itawezekana baada ya hayo, mafanikio yako yataendelea.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo, ee mfalme, sikiliza shauri langu. Achana na dhambi zako na maovu yako, utende haki na kuwaonea huruma waliodhulumiwa; huenda muda wako wa fanaka ukarefushwa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, Ee mfalme, uwe radhi kupokea shauri langu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako uwe na huruma kwa walioonewa. Hivyo itawezekana baada ya hayo mafanikio yako yakaendelea.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, ee mfalme, uwe radhi kupokea shauri langu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako, na uwe na huruma kwa walioonewa. Hivyo itawezekana baada ya hayo, mafanikio yako yakaendelea.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo, mfalme, shauri langu likupendeze: makosa yako yalipe kwa kutenda wongofu! Nayo maovu, uliyoyafanya, yalipe kwa kuwahurumia wanyonge! Hivyo utulivu wako utakuwa wa siku nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akasema kwa sauti: Angalia Babeli, muji mukubwa nilioujenga kwa nguvu zangu ukuwe makao yangu ya kifalme na kwa ajili ya utukufu wangu!