Daniel 4:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jinsi gani zilivyo kubwa ishara zake Mungu! Maajabu yake ni makuu mno! Ufalme wake ni ufalme wa milele; enzi yake yadumu kizazi hata kizazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ishara zake ni kuu kama nini! Na maajabu yake yana nguvu kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; enzi yake hudumu kizazi hadi kizazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jinsi gani zilivyo kubwa ishara zake Mungu! Maajabu yake ni makuu mno! Ufalme wake ni ufalme wa milele; enzi yake yadumu kizazi hata kizazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama jinsi ishara zake zilivyo kuu, jinsi maajabu yake yalivyo na nguvu! Ufalme wake ni ufalme wa milele; enzi yake hudumu kutoka kizazi hadi kizazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ishara zake ni kuu aje, na maajabu yake yana nguvu aje! Ufalme wake ni ufalme wa milele; enzi yake hudumu kutoka kizazi hadi kizazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vistaajabuni vielekezo vyake vilivyo vikuu! Navyo vioja vyake vilivyo vya nguvu! Ufalme wake ni ufalme wa kale na kale, nayo enzi yake ni ya vizazi na vizazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, nikaamuru wenye hekima wote wa Babeli waletwe mbele yangu kusudi wanielezee maana ya ndoto hiyo.