Daniel 4:31 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu alipotamka maneno hayo, sauti kutoka mbinguni ikatamka: “Ewe mfalme Nebukadneza, sikiliza ujumbe huu juu yako! Ufalme umekutoka!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya ufalme yameondolewa kwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu alipotamka maneno hayo, sauti kutoka mbinguni ikatamka: “Ewe mfalme Nebukadneza, sikiliza ujumbe huu juu yako! Ufalme umekutoka!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya kifalme yameondolewa kutoka kwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya ufalme yameondolewa kutoka kwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno hili lilipokuwa lingalimo kinywani mwa mfalme, sauti ikatoka mbinguni kwamba: Wewe mfalme Nebukadinesari, unapashwa habari, ya kuwa ufalme umekwisha kuondoka kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mwisho wa ile miaka saba, mimi Nebukadneza niliinua macho yangu kuangalia juu mbinguni na akili zangu zikanirudilia. Nilimushukuru Mungu Mukubwa na kumuheshimu yeye anayeishi milele: Kwa sababu mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ufalme wake unadumu kwa vizazi vyote.