Daniel 4:32 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utafukuzwa mbali na wanaadamu! Utaishi pamoja na wanyama wa porini kondeni, na utakula majani kama ng'ombe! Utakaa katika hali hiyo kwa muda wa miaka saba, na mwishowe utatambua kwamba Mungu Mkuu ndiye mwenye uwezo juu ya falme za wanaadamu, na humpa ufalme mtu yeyote amtakaye.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utafukuzwa mbali na wanadamu, ukaishi pamoja na wanyama pori, na utakula nyasi kama ng’ombe. Nyakati saba zitapita juu yako, hadi utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala katika falme zote za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utafukuzwa mbali na wanaadamu! Utaishi pamoja na wanyama wa porini kondeni, na utakula majani kama ng'ombe! Utakaa katika hali hiyo kwa muda wa miaka saba, na mwishowe utatambua kwamba Mungu Mkuu ndiye mwenye uwezo juu ya falme za wanaadamu, na humpa ufalme mtu yeyote amtakaye.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utafukuzwa mbali na wanadamu ukaishi pamoja na wanyama pori, utakula manyasi kama ng'ombe. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza ye yote amtakaye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utafukuzwa mbali na wanadamu, ukaishi pamoja na wanyama pori, na utakula manyasi kama ng’ombe. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakufukuza kwenye watu, ukae pamoja na nyama wa porini, tena watakulisha majani kama ng'ombe; miaka saba itapita, ukiwa hivyo, mpaka utakapotambua kwamba: Yule Alioko huko juu ndiye autawalaye ufalme wa watu, naye humpa ampendaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wote wa dunia si kitu; anafanya anavyotaka na viumbe vya mbinguni, na wakaaji wa dunia; hakuna anayeweza kumupinga, au kusema: Unafanya nini?