Daniel 4:33 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara moja jambo hilo juu ya mfalme Nebukadneza likatekelezwa. Alifukuzwa mbali na wanaadamu, akawa anakula majani kama ng'ombe. Alilowa kwa umande wa mbinguni, na nywele zake zikawa ndefu kama manyoya ya tai, na kucha zake kama za ndege.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala nyasi kama ng’ombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni, hadi nywele zake zikakua kama manyoya ya tai, nazo kucha zake kama makucha ya ndege.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara moja jambo hilo juu ya mfalme Nebukadneza likatekelezwa. Alifukuzwa mbali na wanaadamu, akawa anakula majani kama ng'ombe. Alilowa kwa umande wa mbinguni, na nywele zake zikawa ndefu kama manyoya ya tai, na kucha zake kama za ndege.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni mpaka nywele zake zikakua kama manyoya ya tai na kucha zake kama makucha ya ndege.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni mpaka nywele zake zikakua kama manyoya ya tai na kucha zake kama makucha ya ndege.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo neno hilo likamtimilikia Nebukadinesari: akafukuzwa kwenye watu, akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukaloweshwa na umande wa mbinguni, mpaka nywele zake zikawa ndefu kama manyoya ya tai, nazo kucha zake zikawa ndefu kama za ndege.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati uleule akili zangu zikanirudilia; nilirudishiwa vilevile heshima yangu, mamlaka yangu na utukufu wa ufalme wangu. Washauri na wakubwa wangu walikuja kunitafuta, nikarudishwa katika ufalme wangu na kupata heshima kama pale mbele.