Daniel 4:34 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwishoni mwa ile miaka saba, mimi Nebukadneza niliinua macho yangu kutazama juu mbinguni na akili zangu zikanirudia. Nilimshukuru Mungu Mkuu na kumheshimu yeye aishiye milele: Kwa sababu enzi yake ni enzi ya milele, ufalme wake wadumu kizazi hata kizazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwisho wa wakati huo, mimi Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. Utawala wake ni utawala wa milele; ufalme wake hudumu kizazi hadi kizazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwishoni mwa ile miaka saba, mimi Nebukadneza niliinua macho yangu kutazama juu mbinguni na akili zangu zikanirudia. Nilimshukuru Mungu Mkuu na kumheshimu yeye aishiye milele: Kwa sababu enzi yake ni enzi ya milele, ufalme wake wadumu kizazi hata kizazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. Utawala wake ni utawala wa milele; ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. Utawala wake ni utawala wa milele; ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo zilipopita, ndipo, mimi Nebukadinesari nilipoyaelekeza macho yangu mbinguni; ndipo, akili zangu ziliporudi kwangu, nikamtukuza yule Alioko huko juu, nikamsifu na kumheshimu aliye Mwenye uzima wa kale na kale, ukuu wake wa kutawala ni wa kale na kale, nao ufalme wake ni wa vizazi na vizazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sasa, mimi Nebukadneza ninamusifu na kumutukuza na kumuheshimu Mufalme wa mbinguni. Maana matendo yake yote ni ya haki, naye anawashusha wenye kiburi.