Daniel 4:36 — Compare Translations

8 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wakati huo huo akili zangu zikanirudia; nilirudishiwa pia heshima yangu, fahari yangu na utukufu wa ufalme wangu. Washauri na maofisa wangu walikuja kunitafuta, nikarudishwa katika ufalme wangu na kupata heshima kama pale awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, nikarudishiwa heshima yangu na fahari yangu kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme, hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wakati huo huo akili zangu zikanirudia; nilirudishiwa pia heshima yangu, fahari yangu na utukufu wa ufalme wangu. Washauri na maofisa wangu walikuja kunitafuta, nikarudishwa katika ufalme wangu na kupata heshima kama pale awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, heshima yangu na fahari yangu nikarudishiwa kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, nikarudishiwa heshima yangu na fahari yangu kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo, akili zangu ziliporudi kwangu, nikapewa enzi yangu na utukufu wangu, ufalme wangu upate kutukuzwa. Wasemaji wangu wa shaurini na wakuu wangu wakanitafuta, nikarudishwa katika ufalme wangu, ukuu wangu ukaongezwa, ukazidi sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)