Daniel 4:9 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Belteshaza, uliye mkuu wa waganga, nafahamu kuwa roho ya miungu mitakatifu imo ndani yako, na kwamba hakuna fumbo lililo gumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu; niambie maana yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikasema, “Belteshaza, mkuu wa waganga, ninajua kuwa roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako, wala hakuna siri iliyo ngumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu, nifasirie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie njozi za ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Belteshaza, uliye mkuu wa waganga, nafahamu kuwa roho ya miungu mitakatifu imo ndani yako, na kwamba hakuna fumbo lililo gumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu; niambie maana yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilisema, “Belteshaza, mkuu wa waganga, ninajua kuwa Roho ya Miungu Mitakatifu iko ndani yako, wala hakuna siri iliyo ngumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu, nifasirie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilisema, “Belteshaza, mkuu wa waganga, ninajua kuwa roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako, wala hakuna siri iliyo ngumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu, nifasirie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Beltesasari, mkuu wa waandishi, mimi ninakujua, ya kuwa roho ya miungu mitakatifu imo mwako, hakuna fumbo linalokusumbua; hii ni ndoto, niliyoiota, niambie maana yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie njozi za ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Majani yake yalikuwa mazuri. Ulikuwa umejaa matunda mengi yaliyotoshelea kwa kulisha dunia nzima. Nyama wote wa pori walipata kivuli chini yake, na ndege wa anga walikaa katika matawi yake. Viumbe vyote vilipata chakula kutoka muti huo.