Daniel 5:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na kelele za mfalme na wakuu wake, mama mfalme aliingia ukumbini mwa karamu, akasema, “Uishi, ee mfalme! Si lazima mawazo yako yakufadhaishe na kubadilika rangi yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malkia aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi hivyo!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na kelele za mfalme na wakuu wake, mama mfalme aliingia ukumbini mwa karamu, akasema, “Uishi, ee mfalme! Si lazima mawazo yako yakufadhaishe na kubadilika rangi yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malkia aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake alikuja akaingia katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele. Usishtuke! Usibadilike rangi kiasi hicho!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malkia aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi kiasi hicho!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya hayo maneno ya mfalme na ya wakuu wake mamake mfalme akaja mle chumbani, walimonywea, kisha mamake mfalme akasema kwamba: Wewe mfalme na uwe mwenye uzima kale na kale! Mawazo yako yasikustushe, wala uso wako usiwe mwingine!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutokana na kelele za mufalme na wakubwa wake, mama ya mufalme aliingia ndani ya chumba cha karamu, akasema: Uishi milele, ee mufalme! Si lazima mawazo yako yakufazaishe na rangi yako kubadilika.
Recommended Reading