Daniel 5:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika ufalme wako yupo mtu ambaye roho ya miungu mitakatifu imo ndani yake. Wakati wa utawala wa baba yako, mtu huyu alidhihirika kuwa mwenye ujuzi, ufahamu na hekima kama ya miungu. Baba yako, mfalme Nebukadneza, alimfanya kuwa mkuu wa waaguzi, wachawi, Wakaldayo wenye hekima, na wanajimu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yuko mtu katika ufalme wako mwenye roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, naam, mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika ufalme wako yupo mtu ambaye roho ya miungu mitakatifu imo ndani yake. Wakati wa utawala wa baba yako, mtu huyu alidhihirika kuwa mwenye ujuzi, ufahamu na hekima kama ya miungu. Baba yako, mfalme Nebukadneza, alimfanya kuwa mkuu wa waaguzi, wachawi, Wakaldayo wenye hekima, na wanajimu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana Roho ya Miungu Mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimtuma kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika ufalme wako yuko mtu mwenye roho ya miungu mitakatifu, hata siku za baba yako kwake yeye ulioneka mwangaza na utambuzi na ujuzi uliofanana na ujuzi wa miungu, baba yako Nebukadinesari akamweka kuwa mkuu wao waandishi na waaguaji na Wakasidi na wachunguza nyota, kweli baba yako mfalme aliyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika ufalme wako kuna mutu ambaye roho ya miungu mitakatifu iko ndani yake. Wakati wa utawala wa baba yako, mutu huyu alionekana kuwa mwenye ujuzi, ufahamu na hekima kama ya miungu. Baba yako, mufalme Nebukadneza, alimufanya kuwa mukubwa wa waaguzi, wachawi, Wakaldea wenye hekima, na waganga,