Daniel 5:13 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamwuliza: “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa mateka aliowaleta baba yangu mfalme, kutoka nchi ya Yuda?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamuuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Yuda?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Je! Wewe ndiwe Danieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamwuliza: “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa mateka aliowaleta baba yangu mfalme, kutoka nchi ya Yuda?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Uyahudi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamuuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Yuda?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Danieli akapelekwa mbele yake mfalme, mfalme akamwuliza Danieli akisema: Wewe ndiwe Danieli, mmoja wao Wayuda, baba yangu mfalme aliowateka na kuwahamisha kuja huku akiwatoa katika nchi ya Yuda?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Je! Wewe ndiwe Danieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Danieli akaletwa mbele ya mufalme, naye mufalme akamwuliza: Wewe ndiwe Danieli, mumoja wa wafungwa ambao baba yangu mufalme, aliowaleta kutoka inchi ya Yuda?