Daniel 5:16 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, nimesikia kwamba wewe unaweza kueleza vitendawili na kutambua mafumbo. Basi, kama ukifaulu kusoma maandishi haya na kunieleza maana yake, utavishwa mavazi rasmi ya zambarau na kuvishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako. Utapewa nafasi ya tatu katika ufalme huu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu katika ufalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, nimesikia kwamba wewe unaweza kueleza vitendawili na kutambua mafumbo. Basi, kama ukifaulu kusoma maandishi haya na kunieleza maana yake, utavishwa mavazi rasmi ya zambarau na kuvishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako. Utapewa nafasi ya tatu katika ufalme huu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu kutoka juu katika ufalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu katika ufalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini habari zako wewe nimesikia, ya kuwa unaweza kusema maana na kuyavumbua yaliyofunikwa; basi, kama unaweza kuyasoma maandiko haya na kunijulisha maana yao, utavikwa nguo za kifalme, napo shingoni pako utapata mkufu wa dhahabu, tena utakuwa mwenye kutawala wa tatu katika ufalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, nimesikia kwamba wewe unaweza kueleza vitendawili na kutambua mafumbo. Basi, kama ukiweza kusoma maandiko haya na kunielezea maana yake, utavalishwa nguo nzuri ya rangi nyekundu na kuvalishwa mukufu wa zahabu katika shingo lako. Utapewa nafasi ya tatu katika ufalme huu.