Daniel 5:17 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Danieli akamjibu mfalme Belshaza, “Waweza kukaa na zawadi zako ee mfalme au kumpa mtu mwingine. Hata hivyo, ee mfalme, nitakusomea maandishi hayo na kukueleza maana yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Unaweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine thawabu zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Danieli akamjibu mfalme Belshaza, “Waweza kukaa na zawadi zako ee mfalme au kumpa mtu mwingine. Hata hivyo, ee mfalme, nitakusomea maandishi hayo na kukueleza maana yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine ye yote zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa ajili ya mfalme na kumwambia maana yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Waweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine zawadi zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Danieli akamjibu mfalme akisema: Kaa na vipaji vyako! Umpe mwingine matunzo yako! Lakini haya maandiko nitamsomea mfalme, nayo maana yao nitamjulisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Danieli akamujibu mufalme Belsasari: Unaweza kubakia na zawadi zako, ee mufalme, au kumupa mutu mwingine. Hata hivyo, ee mufalme, nitakusomea maandiko hayo na kukuelezea maana yake.