Daniel 5:19 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu ya ukuu aliompa, watu wa makabila yote, mataifa yote na lugha zote walitetemeka na kumwogopa. Nebukadneza aliweza kumuua mtu yeyote aliyetaka na kumwacha hai yeyote aliyetaka. Aliyetaka kumpandisha cheo alimpandisha, aliyetaka kumshusha cheo alimshusha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu ya ukuu aliompa baba yako, watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu ya ukuu aliompa, watu wa makabila yote, mataifa yote na lugha zote walitetemeka na kumwogopa. Nebukadneza aliweza kumuua mtu yeyote aliyetaka na kumwacha hai yeyote aliyetaka. Aliyetaka kumpandisha cheo alimpandisha, aliyetaka kumshusha cheo alimshusha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu ya nafasi ya juu aliyompa baba yako, kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua, wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai, wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha, aliotaka kuwashusha, aliwashusha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu ya nafasi ya juu aliyompa baba yako, kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya ukuu, aliompa, watu wa makabila yote na wa koo zote, wao wote wenye ndimi za watu walitetemeka mbele yake kwa kumwogopa, kwani aliyetaka kumwua, akamwua; naye aliyetaka kumwacha, akamwacha kuwa mzima, naye aliyetaka kumkweza, akamkweza, naye aliyetaka kumnyenyekeza, akamnyenyekeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu ya ukubwa aliomupa, watu wa makabila yote, mataifa yote na luga zote walitetemeka na kumwogopa. Nebukadneza aliweza kumwua mutu yeyote aliyetaka na kumwacha muzima mutu yeyote aliyetaka. Aliyetaka kumupandisha cheo alimupandisha, aliyetaka kumushusha cheo alimushusha.