Daniel 5:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutokana na kunywa divai, mfalme Belshaza akatoa amri vile vyombo vya dhahabu na fedha ambavyo mfalme Nebukadneza, baba yake, alivichukua kutoka hekalu la Yerusalemu, viletwe ili avitumie kunywea divai pamoja na maofisa wake, wake zake na masuria wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Belshaza alipokuwa akinywa divai, aliamuru vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekalu huko Yerusalemu viletwe, ili mfalme na wakuu wake, pamoja na wake zake na masuria wake wapate kuvinywea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutokana na kunywa divai, mfalme Belshaza akatoa amri vile vyombo vya dhahabu na fedha ambavyo mfalme Nebukadneza, baba yake, alivichukua kutoka hekalu la Yerusalemu, viletwe ili avitumie kunywea divai pamoja na maofisa wake, wake zake na masuria wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Belsasari alipokwisha kuonjaonja mvinyo akaagiza, wavilete vile vyombo vya dhahabu na vya fedha, baba yake Nebukadinesari alivyovichukua katika Jumba takatifu huko Yerusalemu, kwamba mfalme na wakuu wake na wakeze na masuria zake wanywee mumo humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutokana na kunywa divai, mufalme Belsasari akatoa amri kwamba vile vyombo vya zahabu na feza ambavyo baba yake mufalme Nebukadneza alivyokamata kutoka hekalu la Yerusalema, viletwe kusudi avitumie kwa kunywea divai pamoja na wakubwa wake, wanawake wake na wahabara wake.