Daniel 5:21 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alifukuzwa mbali na wanaadamu, akili yake ikafanywa kama ya mnyama, akaishi na pundamwitu, akawa anakula majani kama ng'ombe. Alinyeshewa mvua mwilini mpaka alipotambua kwamba Mungu Mkuu ndiye atawalaye falme za wanaadamu, naye humweka mfalme yeyote amtakaye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu; akala majani kama ng’ombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, hadi alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala katika falme zote za wanadamu, na kwamba humtawaza juu yao yeyote amtakaye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alifukuzwa mbali na wanaadamu, akili yake ikafanywa kama ya mnyama, akaishi na pundamwitu, akawa anakula majani kama ng'ombe. Alinyeshewa mvua mwilini mpaka alipotambua kwamba Mungu Mkuu ndiye atawalaye falme za wanaadamu, naye humweka mfalme yeyote amtakaye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu, akala majani kama ng'ombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, mpaka alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala juu ya falme za wanadamu na kwamba humtawaza juu yao ye yote amtakaye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu, akala majani kama ng’ombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, mpaka alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala juu ya falme za wanadamu na kwamba humtawaza juu yao yeyote amtakaye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akafukuzwa kwenye watu, wakauwazia moyo wake kuwa kama wa nyama wa porini, akakaa pamoja na punda wa mwituni, wakamlisha majani kama ng'ombe, mwili wake ukaloweshwa na umande wa mbinguni, mpaka alipotambua, ya kuwa Mungu Alioko huko juu ndiye autawalaye ufalme wa watu, naye ampendaye humkweza, aupate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifukuzwa mbali na wanadamu, akili yake ikafanywa kama ya nyama, akaishi na punda wa pori, akakuwa anakula majani kama ngombe, na kulowanishwa na umande wa mbinguni mpaka alipotambua kwamba Mungu Mukubwa ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye anamupa ufalme ule mutu yeyote anayemutaka.