Daniel 5:23 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Badala yake umejikuza mwenyewe dhidi ya Bwana wa mbinguni: Umeleta vyombo vya nyumba yake Mungu ukavitumia kunywea divai, wewe, maofisa wako, wake zako na masuria wako, na kuisifu miungu iliyotengenezwa kwa fedha, dhahabu, shaba, chuma, miti na mawe; miungu ambayo haioni, haisikii wala haijui lolote. Lakini Mungu, ambaye uhai wako u mkononi mwake, na njia zako zi wazi mbele yake, hukumheshimu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, pamoja na wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea divai. Uliisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Badala yake umejikuza mwenyewe dhidi ya Bwana wa mbinguni: umeleta vyombo vya nyumba yake Mungu ukavitumia kunywea divai, wewe, maofisa wako, wake zako na masuria wako, na kuisifu miungu iliyotengenezwa kwa fedha, dhahabu, shaba, chuma, miti na mawe; miungu ambayo haioni, haisikii wala haijui lolote. Lakini Mungu, ambaye uhai wako u mkononi mwake, na njia zako zi wazi mbele yake, hukumheshimu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha, ya dhahabu, ya shaba, ya chuma, ya miti na ya mawe, miungu ambayo haiwezi kuona au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukamwinukia Bwana wa mbinguni, ukavitaka hivi vyombo vya Nyumba yake, wakutolee, wewe unywee mumo humo mvinyo pamoja na wake zako na masuria zako na wakuu wako, mkaisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba na ya chuma na ya miti na ya mawe isiyoona, isiyosikia, isiyojua kitu; lakini hukumtukuza Mungu azishikaye pumzi zako mkononi mwake, naye ndiye azilinganyaye njia zako zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali pake umejitukuza mwenyewe mbele ya Bwana wa mbinguni: umeleta vyombo vya nyumba ya Mungu ukavitumia kwa kunywea divai, wewe, wakubwa wako, wanawake wako na wahabara wako, na kuisifu miungu iliyotengenezwa na feza, zahabu, shaba, chuma, miti na mawe; miungu ambayo haioni, haisikii wala haijui jambo lolote. Lakini Mungu, ambaye uzima wako uko katika mukono wake, na njia zako ziko wazi mbele yake, haukumuheshimu!