Daniel 5:29 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, mfalme Belshaza akaamuru Danieli avishwe mavazi rasmi ya zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni. Ikatangazwa kuwa Danieli atashikilia nafasi ya tatu katika ufalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, mfalme Belshaza akaamuru Danieli avishwe mavazi rasmi ya zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni. Ikatangazwa kuwa Danieli atashikilia nafasi ya tatu katika ufalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu kutoka juu katika ufalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Belsasari akatoa amri, wakamvika Danieli nguo za kifalme na mkufu wa dhahabu shingoni, wakatangaza, ya kuwa atakuwa mwenye kutawala wa tatu katika ufalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pale pale, mufalme Belsasari akaamuru kwamba Danieli avalishwe nguo nzuri nyekundu na mukufu wa zahabu katika shingo. Ikatangazwa kwamba Danieli atakamata sasa nafasi ya tatu katika ufalme.