Daniel 5:3 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, vile vyombo vya dhahabu na fedha vilivyochukuliwa hekaluni Yerusalemu vikaletwa. Mfalme, maofisa wake, wake zake na masuria wake wakavitumia kunywea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, pamoja na wake zake na masuria wake wakavinywea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, vile vyombo vya dhahabu na fedha vilivyochukuliwa hekaluni Yerusalemu vikaletwa. Mfalme, maofisa wake, wake zake na masuria wake wakavitumia kunywea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka katika Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wakavileta vile vyombo vya dhahabu, walivyovichukua katika Jumba takatifu la Mungu huko Yerusalemu, mfalme na wakuu wake na wakeze na masuria zake wakanywea mumo humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, vile vyombo vya zahabu na feza vilivyokamatwa katika hekalu kule Yerusalema vikaletwa. Mufalme, wakubwa wake, wanawake wake na wahabara wake wakavitumia kwa kunywea.