Daniel 5:7 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Belshaza akapaaza sauti waletwe wachawi, Wakaldayo wenye hekima na wanajimu waletwe. Walipoletwa, mfalme akawaambia wenye hekima hao wa Babuloni, “Yeyote atakayesoma maandishi haya na kunijulisha maana yake, atavishwa mavazi rasmi ya zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, na kupewa nafasi ya tatu katika ufalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waaguzi waletwe, naye akawaambia hao wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Belshaza akapaaza sauti waletwe wachawi, Wakaldayo wenye hekima na wanajimu waletwe. Walipoletwa, mfalme akawaambia wenye hekima hao wa Babuloni, “Yeyote atakayesoma maandishi haya na kunijulisha maana yake, atavishwa mavazi rasmi ya zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, na kupewa nafasi ya tatu katika ufalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Ye yote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake, atavikwa nguo za zambarau na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa tatu kutoka juu katika ufalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akalia kwa sauti kuu, wamletee waaguaji na Wakasidi na wachunguza nyota, kisha mfalme akawaambia hao wajuzi wa Babeli akisema: Mtu ye yote atakayeyasoma maandiko haya na kunieleza maana yake atavikwa nguo za kifalme, napo shingoni pake atapata mkufu wa dhahabu, naye atakuwa mwenye kutawala wa tatu katika ufalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Belsasari akaamuru kwa sauti kwamba wachawi, Wakaldea wenye hekima na waaguzi waletwe. Walipoletwa, mufalme akawaambia wenye hekima hao wa Babeli: Yeyote atakayesoma maandiko haya na kunijulisha maana yake, atavalishwa nguo nzuri nyekundu za kifalme na mukufu wa zahabu katika shingo lake, na kupewa nafasi ya tatu katika ufalme.