Daniel 6:11 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wale waliofanya mpango dhidi ya Danieli waliingia ndani, wakamkuta Danieli akiomba dua na kumsihi Mungu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo watu hawa wakaenda kama kikundi na kumkuta Danieli akiomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wale waliofanya mpango dhidi ya Danieli waliingia ndani, wakamkuta Danieli akiomba dua na kumsihi Mungu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo watu hawa wakamwendea kama kikundi na kumkuta Danieli anaomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo watu hawa wakaenda kama kikundi na kumkuta Danieli akiomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wale waume wakamwendea kwa kushangilia mioyoni, wakamwona Danieli, alivyomwomba Mungu wake na kumlalamikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Danieli alipojua kwamba ile sheria imetiwa sahihi, alirudi kwa nyumba yake kwenye gorofi katika chumba chake kilichokuwa na madirisha yaliyofunguka kuelekea Yerusalema. Humo, Danieli, kama ilivyokuwa kawaida yake, alipiga magoti mara tatu kila siku kwa kuomba na kumushukuru Mungu wake.