Daniel 6:13 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamwambia mfalme, “Yule Danieli aliye mmoja wa mateka kutoka nchi ya Yuda hakuheshimu wewe mfalme wala haitii amri uliyotia sahihi. Yeye anasali mara tatu kila siku.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa mahamisho kutoka Yuda, hakuheshimu, ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Bado anaomba mara tatu kwa siku.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamwambia mfalme, “Yule Danieli aliye mmoja wa mateka kutoka nchi ya Yuda hakuheshimu wewe mfalme wala haitii amri uliyotia sahihi. Yeye anasali mara tatu kila siku.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa watu wa uhamisho kutoka Yuda hakuheshimu, Ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Angalia anaomba mara tatu kwa siku.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa mahamisho kutoka Yuda, hakuheshimu, ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Bado anaomba mara tatu kwa siku.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakamjibu mfalme na kumwambia: Danieli aliye mmoja wao Wayuda waliotekwa na kuhamishwa kuja huku, hakuchi, wala haishiki amri yako, mfalme, ya kutisha watu, uliyoiandika, ila huomba maombo yake kila siku mara tatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, walikwenda kwa mufalme na kumushitaki Danieli kwa kutumia ile sheria, wakisema: Mufalme Dario, haukutia sahihi kwenye sheria kwamba kwa muda wa siku makumi tatu hakuna mutu yeyote atakayeruhusiwa kuomba kitu chochote, kwa mungu yeyote, au kwa mutu yeyote isipokuwa kutoka kwako wewe, ee mufalme, na kwamba yeyote atakayevunja sheria hii atatumbukizwa katika pango la simba? Mufalme akaitikia: Hivi ndivyo inavyokuwa kulingana na sheria ya Wamedi na Wapersi ambayo haiwezi kuvunjika.