Daniel 6:14 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme aliposikia maneno hayo, alisikitika sana. Akajitahidi sana kupata njia ya kumwokoa Danieli. Aliendelea kujaribu mpaka jua likatua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme aliposikia hili, akahuzunika mno. Akakusudia kumwokoa Danieli, hivyo akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme aliposikia maneno hayo, alisikitika sana. Akajitahidi sana kupata njia ya kumwokoa Danieli. Aliendelea kujaribu mpaka jua likatua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mfalme aliposikia hili, akahuzunishwa mno, akakusudia kumwokoa Danieli, naye akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mfalme aliposikia hili, akahuzunika mno. Akakusudia kumwokoa Danieli, hivyo akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme alipolisikia neno hili, halikumpendeza kabisa, akafikiri moyoni, jinsi atakavyomwokoa Danieli; mpaka jua likiingia, akawa akihangaikia mizungu ya kumponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamwambia mufalme: Yule Danieli anayekuwa mumoja wa wafungwa kutoka inchi ya Yuda hakuheshimu wewe mufalme wala amri uliyotia sahihi. Anafanya maombi yake mara tatu kila siku.