Daniel 6:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale watu wakamwendea mfalme Dario kwa pamoja na kumwambia, “Ee mfalme, ujue kuwa hakuna sheria wala amri yoyote ya Wamedi na Wapersi inayoweza kubatilishwa baada ya kuwekwa na mfalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wale watu wakamwendea mfalme kama kikundi na kumwambia, “Ee mfalme, kumbuka kwamba kulingana na sheria ya Wamedi na Waajemi, hakuna amri wala sheria ambayo mfalme ameitoa inayoweza kubadilishwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale watu wakamwendea mfalme Dario kwa pamoja na kumwambia, “Ee mfalme, ujue kuwa hakuna sheria wala amri yoyote ya Wamedi na Wapersi inayoweza kubatilishwa baada ya kuwekwa na mfalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wale watu wakamwendea mfalme kama kikundi na kumwambia, “Ee mfalme, kumbuka kwamba kulingana na sheria ya Wamedi na Waajemi hakuna amri wala sheria ambayo mfalme ameitoa inayoweza kubadilishwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wale watu wakamwendea mfalme kama kikundi na kumwambia, “Ee mfalme, kumbuka kwamba kulingana na sheria ya Wamedi na Waajemi, hakuna amri wala sheria ambayo mfalme ameitoa inayoweza kubadilishwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wale waume walipomwendea mfalme na kushangilia mioyoni, wakamwambia mfalme: Unajua, mfalme, ya kuwa kwa maongozi yetu Wamedi na Wapersia haiwezekani kugeuza katazo wala amri, mfalme aliyoitoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme aliposikia maneno hayo, alisikitika sana. Akafanya nguvu yake yote kwa kutafuta njia ya kumwokoa Danieli. Aliendelea kujaribu mpaka jua likatua.