Daniel 6:16 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme Dario akatoa amri, naye Danieli akaletwa na kutupwa katika pango la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako ambaye unamtumikia daima, na akuokoe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme Dario akatoa amri, naye Danieli akaletwa na kutupwa katika pango la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako ambaye unamtumikia daima, na akuokoe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, na wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipoagiza, wamlete Danieli, wamtupe pangoni mwa simba. Naye akamwambia Danieli: Mungu wako, unayemtumikia pasipo kukoma, ndiye atakayekuokoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu kwa pamoja wakamwendea mufalme Dario na kumwambia: Ee mufalme, ujue kwamba hakuna sheria wala amri yoyote ya Wamedi na Wapersi inayoweza kubadilishwa kisha kuwekwa na mufalme.