Daniel 6:17 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jiwe likaletwa na kuwekwa mlangoni mwa lile pango. Mfalme akalipiga mhuri wake binafsi na ule wa wakuu wake, ili uamuzi kuhusu Danieli usibatilishwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jiwe likaletwa na kuwekwa kwenye mlango wa tundu, naye mfalme akalitia muhuri kwa pete yake mwenyewe pamoja na kwa pete za wakuu wake, ili hali ya Danieli isiweze kubadilishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jiwe likaletwa na kuwekwa mlangoni mwa lile pango. Mfalme akalipiga mhuri wake binafsi na ule wa wakuu wake, ili uamuzi kuhusu Danieli usibatilishwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jiwe likaletwa na kuwekwa kwenye mdomo wa tundu, naye mfalme akalitia muhuri kwa pete yake mwenyewe pamoja na kwa pete za wakuu wake, ili kwamba hali ya Danieli isiweze kubadilishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jiwe likaletwa na kuwekwa kwenye mdomo wa tundu, naye mfalme akalitia muhuri kwa pete yake mwenyewe pamoja na kwa pete za wakuu wake, ili hali ya Danieli isiweze kubadilishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakaletwa jiwe moja, likawekwa juu hapo pa kuliingilia lile pango, mfalme akalitia muhuri kwa pete yake yenye muhuri na kwa pete ya wakuu wake yenye muhuri, jambo la Danieli lisigeuzwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme Dario akatoa amri, naye Danieli akaletwa na kutupwa katika pango la simba. Mufalme akamwambia Danieli: Mungu wako ambaye unamutumikia siku zote akuokoe.