Daniel 6:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwateua pia wakuu watatu, Danieli akiwa mmojawapo, wawasimamie wale wakuu wengine na maslahi ya mfalme, asije akapata hasara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pamoja na wasimamizi watatu juu yao, Danieli akiwa mmoja wao. Wakuu walitoa hesabu kwa wasimamizi hao ili mfalme asipate hasara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwateua pia wakuu watatu, Danieli akiwa mmojawapo, wawasimamie wale wakuu wengine na maslahi ya mfalme, asije akapata hasara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao nao akawapatia wakuu watatu, mmoja wao akawa Danieli; wale watawala nchi hawakuwa na budi kuwatolea hawa hesabu, mfalme asipotelewe na mali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Dario aliamua kuweka wakubwa mia moja na makumi mbili kwa kusimamia mambo ya ufalme.