Daniel 6:20 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipofika karibu akamwita Danieli kwa sauti ya huzuni, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima ameweza kukuokoa na simba hawa?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokaribia lile tundu, mfalme akamwita Danieli kwa sauti ya uchungu: “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako, unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa kwa simba?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipofika karibu akamwita Danieli kwa sauti ya huzuni, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima ameweza kukuokoa na simba hawa?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati alipokaribia lile tundu, alimwita Danieli kwa sauti ya uchungu, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je, Mungu wako unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa na simba hawa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati alipokaribia lile tundu, akamwita Danieli kwa sauti ya uchungu, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa kwa simba?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipolifikia hilo pango karibu, akamwita Danieli na kupaza sauti kiwogawoga, yeye mfalme akasema na kumwuliza Danieli: Danieli uliye mtumishi wake Mungu aliye Mwenye uzima! Je? Mungu wako, unayemtumikia pasipo kukoma, ameweza kukuokoa katika simba?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilipokuwa asubui mapema, mufalme Dario aliamuka, akaenda kwa haraka kwenye pango la simba.