Daniel 6:22 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lo lote baya mbele yako, Ee mfalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu ametuma malaika wake, akavifumba vinywa vya simba, hawakuniumiza, kwa kuwa mbele yake nimeonekana kuwa mtu asiyekosa; hata mbele yako, mfalme, hakuna kiovu, nilichokifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Danieli akamujibu mufalme: Uishi milele, ee mufalme!