Daniel 6:23 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo mfalme akafurahi sana; akaamuru Danieli atolewe pangoni. Basi wakamtoa, naye alikuwa hajadhurika hata kidogo, kwa sababu alimtegemea Mungu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Mfalme akafurahi mno, akatoa amri Danieli atolewe kutoka kwa lile tundu. Danieli alipotolewa kutoka kwa lile tundu, hakukutwa na jeraha lolote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo mfalme akafurahi sana; akaamuru Danieli atolewe pangoni. Basi wakamtoa, naye alikuwa hajadhurika hata kidogo, kwa sababu alimtegemea Mungu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akafurahi mno naye akatoa amri Danieli atolewe kwenye lile tundu. Danieli alipotolewa katika lile tundu, hakukutwa na jeraha lo lote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akafurahi mno, naye akatoa amri Danieli atolewe kutoka kwa lile tundu. Danieli alipotolewa kutoka kwa lile tundu, hakukutwa na jeraha lolote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipomfurahia sanasana, akaagiza kumtoa Danieli pangoni; basi, Danieli alipokwisha kutolewa mle pangoni hamkuonekana mwilini mwake kidonda cho chote, kwani alimtumaini Mungu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu wangu alileta malaika wake kwa kufunga vinywa vya simba hawa, nao hawakunizuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina kosa lolote mbele yake na wala sijafanya jambo lolote baya mbele yako.