Daniel 6:24 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akaamuru wale watu waliomchongea Danieli wakamatwe, nao wakatupwa ndani ya lile pango la simba pamoja na wake zao na watoto wao. Nao, hata kabla hawajagusa chini, simba waliwashambulia na kuivunjavunja mifupa yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya mfalme, wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akaamuru wale watu waliomchongea Danieli wakamatwe, nao wakatupwa ndani ya lile pango la simba pamoja na wake zao na watoto wao. Nao, hata kabla hawajagusa chini, simba waliwashambulia na kuivunjavunja mifupa yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa amri ya mfalme wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa amri ya mfalme, wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme akaagiza kuwaleta wale waume waliomchongea Danieli, wawatupe humo pangoni mwa simba, wao na wana wao na wake zao. Walipokuwa hawajafika pangoni chini, simba wakawakamata, wakawavunja mifupa yao yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo mufalme akafurahi sana; akaamuru kwamba wamwondoe Danieli toka ndani ya pango. Basi wakamwondoa, naye hakuonekana na alama hata kidogo ya kidonda, kwa sababu alimutegemea Mungu wake.