Daniel 6:25 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha duniani kote: “Mafanikio yawe kwenu sana!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa na watu wa kila lugha katika nchi yote: “Ninyi na mstawi sana!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa, na watu wa kila lugha katika nchi yote: “Ninyi na mstawi sana!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote na wa koo zote, wao wote wenye ndimi za watu waliokaa katika nchi yote nzima, kwamba: Utengemano wenu na uwe mwingi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akaamuru wale watu waliomuchongea Danieli wakamatwe, nao wakatupwa ndani ya lile pango la simba pamoja na wake wao na watoto wao. Nao, hata mbele hawajagusa chini, simba waliwashambulia na kuivunjavunja mifupa yao.