Daniel 6:26 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitatoa amri kwamba watu wote katika ufalme wangu ni lazima wamwogope na kumcha Mungu wa Danieli. “Yeye ni Mungu aliye hai, aishiye milele; ufalme wake kamwe hauwezi kuangamizwa, utawala wake hauna mwisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Natoa amri hii, kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu, lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli. “Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai, naye hudumu milele. Ufalme wake hautaangamizwa, nao utawala wake hauna mwisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitatoa amri kwamba watu wote katika ufalme wangu ni lazima wamwogope na kumcha Mungu wa Danieli. “Yeye ni Mungu aliye hai, aishiye milele; ufalme wake kamwe hauwezi kuangamizwa, utawala wake hauna mwisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Natoa amri hii kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli. “Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai naye hudumu milele, ufalme wake hautaangamizwa, nao utawala wake kamwe hauna mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Natoa amri hii, kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu, lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli. “Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai, naye hudumu milele, ufalme wake hautaangamizwa, nao utawala wake hauna mwisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwangu inatoka amri hii: Katika ufalme wangu wote, ninaoutawala, watu sharti watetemeke mbele yake Mungu wa Danieli kwa kumwogopa. Kwani yeye ndiye Mungu Mwenye uzima akaaye kale na kale, ufalame wake hauangamii, kutawala kwake hakuna mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na luga zote katika dunia: Ninawatakia amani kwa wingi.