Daniel 6:27 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye hukomboa na kuokoa, hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani, maana amemwokoa Danieli makuchani mwa simba.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huponya na kuokoa; hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani. Amemwokoa Danieli kutoka nguvu za simba.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye hukomboa na kuokoa, hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani, maana amemwokoa Danieli makuchani mwa simba.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huponya na kuokoa: hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani. Amemponya Danieli kutoka katika nguvu za simba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huponya na kuokoa; hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani. Amemwokoa Danieli kutoka nguvu za simba.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye huokoa na kuponya, hufanya vielekezo na vioja mbinguni na nchini, naye ndiye aliyemwokoa Danieli mikononi mwa simba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninatoa amri katika ufalme wangu kwamba watu wote wanapaswa kumwogopa na kumuheshimu Mungu wa Danieli. Yeye ni Mungu Mwenye Uzima, anayeishi milele; ufalme wake hauwezi kuangamizwa hata kidogo, utawala wake hauna mwisho.