Daniel 6:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muda si muda, Danieli akadhihirika kuwa bora kuliko wale wasimamizi wengine na wakuu wote kwa kuwa alikuwa na roho njema. Hivyo mfalme akanuia kumpa uongozi wa ufalme wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Danieli alijidhihirisha miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee, hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muda si muda, Danieli akadhihirika kuwa bora kuliko wale wasimamizi wengine na wakuu wote kwa kuwa alikuwa na roho njema. Hivyo mfalme akanuia kumpa uongozi wa ufalme wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Danieli alijidhihirisha mwenyewe, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Danieli alijidhihirisha, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, huyu Danieli alipowashinda wakuu wenziwe na watawala nchi, kwa kuwa Roho iliyo kuu ilikuwa mwake, naye mfalme akafikiri kumpa ufalme wote, auangalie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliweka vilevile wakubwa watatu, Danieli akiwa mumoja kati yao, wawasimamie wale wakubwa wengine katika uongozi kusudi mufalme asipatwe na hasara.