Daniel 6:4 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wakuu pamoja na maliwali wakatafuta kisingizio cha kumshtaki Danieli kuhusu mambo ya ufalme, lakini hawakuweza kupata sababu ya kumlaumu, wala kosa lolote, kwani Danieli alikuwa mwaminifu. Hakupatikana na kosa, wala hatia yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipofahamu hilo, wasimamizi na wakuu wakajaribu kutafuta sababu za kumshtaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu, wala hakupatikana na upotovu au uzembe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wakuu pamoja na maliwali wakatafuta kisingizio cha kumshtaki Danieli kuhusu mambo ya ufalme, lakini hawakuweza kupata sababu ya kumlaumu, wala kosa lolote, kwani Danieli alikuwa mwaminifu. Hakupatikana na kosa, wala hatia yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hili, wakuu na wasimamizi wakajaribu kutafuta sababu za kumshitaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu na wala hakupatikana na upotovu wala uzembe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipofahamu hilo, wakuu na wasimamizi wakajaribu kutafuta sababu za kumshtaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu, wala hakupatikana na upotovu au uzembe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wakuu na watawala nchi wakatafuta jambo la kumwonea Danieli kwamba: anaukosea ufalme, lakini hawakupata jambo lo lote la kumwonea kwamba: amefanya vibaya, kwa kuwa alikuwa mwelekevu, halikuonekana kwake kosa lo lote wala tendo baya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Danieli akaonekana kuwa bora kuliko wale wasimamizi wengine na wakubwa wote kwa maana alikuwa na roho njema. Hivyo mufalme akakusudia kumupa uongozi wa ufalme wote.