Daniel 6:5 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo wakapatana hivi: “Hatutapata kisingizio chochote cha kumshtaki Danieli isipokuwa kama kisingizio hicho kitakuwa kinahusu sheria ya Mungu wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwishoni watu hawa wakasema, “Kamwe hatutapata msingi wa mashtaka dhidi ya huyu Danieli, isipokuwa iwe inahusiana na sheria ya Mungu wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo wakapatana hivi: “Hatutapata kisingizio chochote cha kumshtaki Danieli isipokuwa kama kisingizio hicho kitakuwa kinahusu sheria ya Mungu wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwishoni watu hawa walisema, “Kamwe hatutapata msingi kwa ajili ya mashtaka dhidi ya mtu huyu Danieli isipokuwa kile kinachohusiana na sheria ya Mungu wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwishoni watu hawa walisema, “Kamwe hatutapata msingi wa mashtaka dhidi ya huyu Danieli isipokuwa iwe inahusiana na Torati ya Mungu wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, hao waume waliposema: Kwake Danieli hatutapata jambo lo lote la kumwonea, tusipomwonea kwa hivyo, anavyomcha Mungu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wakubwa pamoja na maliwali wakatafuta kisingizio cha kumushitaki Danieli juu ya mambo ya ufalme, lakini hawakuweza kupata sababu ya kumushitaki, wala kosa lolote, maana Danieli alikuwa mwaminifu. Hakupatikana na kosa, wala ubaya wowote.