Daniel 6:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, ee mfalme Dario, utoe amri hiyo na kuitia hati sahihi yako ili isibadilishwe. Nayo itakuwa sheria ya Wamedi na Wapersi, sheria ambayo haibatilishwi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa, ee mfalme, toa amri na uiandike ili isiweze kubadilishwa: kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, ee mfalme Dario, utoe amri hiyo na kuitia hati sahihi yako ili isibadilishwe. Nayo itakuwa sheria ya Wamedi na Wapersi, sheria ambayo haibatilishwi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa, Ee mfalme, toa amri na uiandike ili kwamba isiweze kubadilishwa, kwa kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa, ee mfalme, toa amri na uiandike ili isiweze kubadilishwa: kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa, mfalme, itoe amri hii ya huo mwiko, kaiandike kitabuni, isiwezekane kugeuzwa kwa hivyo, maongozi ya Wamedi na ya Wapersia yalivyo, wala isitanguliwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi wakubwa uliotuweka, wasimamizi, maliwali, washauri na wakubwa wa majimbo, wote tumepatana kwamba inafaa, ee mufalme, utoe amri na kuhakikisha kwamba inafuatwa kikamilifu. Amuru kwamba kwa muda wa siku makumi tatu kusikuwe mutu yeyote atakayeruhusiwa kuomba kitu chochote kwa mungu yeyote au kwa mutu yeyote, isipokuwa kutoka kwako wewe, ewe mufalme. Mutu yeyote atakayevunja sheria hii atupwe katika pango la simba.