Daniel 7:1 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa mfalme Belshaza wa Babuloni, Danieli aliota ndoto na kuona maono akiwa amelala kitandani mwake. Aliiandika ndoto yake hii:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita mawazoni mwake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa mfalme Belshaza wa Babuloni, Danieli aliota ndoto na kuona maono akiwa amelala kitandani mwake. Aliiandika ndoto yake hii:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita katika akili yake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita mawazoni yake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Belsasari, mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, akaona maono kwa macho yake alipolala kitandani. Kisha akaiandika hiyo ndoto na kuyasema mambo yake makuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa mufalme Belsasari wa Babeli, Danieli aliota ndoto na kuona maono akiwa amelala katika kitanda chake. Akaandika ndoto yake hii: