Daniel 7:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kutokana na maneno ya kujigamba yaliyokuwa yanasemwa na ile pembe, nikatazama. Nikiwa natazama, huyo mnyama wa nne aliuawa, mwili wake ukaharibiwa na kutolewa uchomwe moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia hadi yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kutokana na maneno ya kujigamba yaliyokuwa yanasemwa na ile pembe, nikatazama. Nikiwa natazama, huyo mnyama wa nne aliuawa, mwili wake ukaharibiwa na kutolewa uchomwe moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia mpaka yule mnyama alipochinjwa na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto unaowaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia mpaka yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawa nikitazama hapohapo kwa ajili ya makelele makubwa, ambayo iliyapiga ile pembe isemayo; nikatazama vivyo hivyo, mpaka yule nyama akiuawa, mwili wake ukaangamizwa ukitupwa motoni, uteketezwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutokana na maneno ya kujivuna yaliyokuwa yanasemwa na ile pembe, nikaendelea kuangalia. Nikaona yule nyama wa ine akiuawa, mwili wake ukaharibiwa na kutolewa uchomwe kwa moto.