Daniel 7:14 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme, ili watu wa makabila yote, mataifa yote na lugha zote wamtumikie. Utawala wake ni wa milele na ufalme wake kamwe hautaangamizwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu; nao watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme, ili watu wa makabila yote, mataifa yote na lugha zote wamtumikie. Utawala wake ni wa milele na ufalme wake kamwe hautaangamizwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu, watu, kabila zote za mataifa na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu; nao watu wa kabila zote, mataifa, na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akapewa nguvu za kutawala na macheo na ufalme, watu wa makabila yote na wa koo zote, wao wote wenye ndimi za watu wamtumikie, nguvu zake za kutawala ni za kale na kale, hazina mwisho, hata ufalme wake hautaangamia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme, kusudi watu wa makabila yote, mataifa yote na luga zote wamutumikie. Utawala wake ni wa milele na ufalme wake hautaangamizwa hata kidogo.