Daniel 7:19 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha nikataka nielezwe juu ya yule mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti kabisa na wale wengine, wa ajabu na wa kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma na makucha yake ya shaba. Aliyatumia meno hayo kula na kuvunjavunja, na mabaki aliyakanyagakanyaga kwa nyayo zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, aliyekuwa tofauti na wale wengine wote, tena wa kutisha sana, na meno yake ya chuma na makucha ya shaba: mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chochote kilichosalia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha nikataka nielezwe juu ya yule mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti kabisa na wale wengine, wa ajabu na wa kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma na makucha yake ya shaba. Aliyatumia meno hayo kula na kuvunjavunja, na mabaki aliyakanyagakanyaga kwa nyayo zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, ambaye alikuwa tofauti na wale wengine wote tena wa kutisha mwenye meno ya chuma na makucha ya shaba, mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake na kukanyaga cho chote kilichosalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, ambaye alikuwa tofauti na wale wengine wote, tena wa kutisha sana, na meno yake ya chuma na makucha ya shaba: mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chochote kilichosalia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikamwuliza tena maana ya kweli ya nyama wa nne aliyekuwa mwingine kabisa, asifanane na wenzake wote, aliyestusha kabisa kwa kuwa mwenye meno ya chuma na mwenye kucha za shaba, aliyekula na kuvunjavunja, nayo yaliyosalia aliyakanyagakanyaga kwa miguu yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikataka nielezwe juu ya yule nyama wa ine, ambaye alikuwa tofauti kabisa na wale wengine, wa kutisha sana, mwenye meno ya chuma na makucha ya shaba, aliyekula na kuvunjavunja, na kukanyagakanyaga yaliyobaki.