Daniel 7:20 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aidha nilitaka nielezwe juu ya zile pembe kumi alizokuwa nazo kichwani mwake, na ule upembe mmoja ambao kabla haujaota, zilingoka pembe tatu; upembe uliokuwa na macho na kinywa ambacho kilitamka maneno ya kujigamba, na ambao ulionekana kuwa mkubwa kuliko pembe nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake, na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho kuliko zile nyingine, na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aidha nilitaka nielezwe juu ya zile pembe kumi alizokuwa nazo kichwani mwake, na ule upembe mmoja ambao kabla haujaota, ziling'oka pembe tatu; upembe uliokuwa na macho na kinywa ambacho kilitamka maneno ya kujigamba, na ambao ulionekana kuwa mkubwa kuliko pembe nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho zaidi kuliko zile nyingine na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake, na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho zaidi kuliko zile nyingine, na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikauliza nayo maana ya zile pembe kumi za kichwani pake, nayo maana ya ile pembe nyingine, ambayo mbele yake zikang'oka pembe tatu, iliyokuwa yenye macho kama ya mtu, tena yenye kinywa kilichosema makuu; naye alionekana kuwa mkubwa kuliko wenziwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile nilitaka nielezwe juu ya zile pembe kumi alizokuwa nazo juu ya kichwa chake, na ile pembe moja iliyoota na pembe zingine tatu zilizoanguka mbele yake, ndiyo ile pembe iliyokuwa na macho na kinywa ambacho kilisema maneno ya kujivuna, na ambayo ilionekana kuwa kubwa kuliko pembe zingine.