Daniel 7:23 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nikaelezwa hivi: ‘Yule mnyama wa nne ni ufalme wa nne utakaokuwako duniani. Ufalme huo utakuwa tofauti na falme nyingine, nao utaiangamiza dunia nzima. Utaibwaga chini na kuipasua vipandevipande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote, nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nikaelezwa hivi: ‘Yule mnyama wa nne ni ufalme wa nne utakaokuwako duniani. Ufalme huo utakuwa tofauti na falme nyingine, nao utaiangamiza dunia nzima. Utaibwaga chini na kuipasua vipandevipande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote, nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia haya: Huyo nyama wa nne ndio ufalme wa nne utakaokuwa katika nchi, nao utakuwa mwingine, usifanane na ufalme wote, utaila nchi yote nzima, utaiponda kwa kuikanyagakanyaga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilielezwa hivi: Yule nyama wa ine ni ufalme wa ine utakaokuwa katika dunia. Ufalme huo utakuwa tofauti na falme zingine, nao utaiangamiza dunia nzima. Utaiangusha chini na kuipasua vipandevipande.