Daniel 7:25 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo atamkufuru Mungu Mkuu na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha nyakati na sheria zao, na watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwatesa watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo atamkufuru Mungu Mkuu na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha nyakati na sheria zao, na watakatifu watatiwa mikononi mwake kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili sikukuu zao takatifu pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena atasema maneno ya kumbeza Alioko huko juu, nao watakatifu wake Alioko huko juu atawapondaponda; tena atajipa moyo wa kuzigauza sikukuu, atoe nyingine, hata maongozi, atoe mengine. Nao watakatifu watatiwa mikononi mwake kipande cha siku na vipande viwili vya siku na nusu ya kipande cha siku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo atasema maneno ya kujivuna mbele ya Mungu Mukubwa na kuwatesa watakatifu wake. Atajaribu kubadilisha sikukuu na sheria zao, na watakatifu watatiwa katika mikono yake kwa muda wa miaka mitatu na nusu.