Daniel 7:27 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ufalme, utawala na ukuu wa falme zote duniani watapewa watu wa watakatifu wa Mungu Mkuu. Ufalme wao utakuwa wa kudumu milele, na tawala zote zitawatumikia na kuwatii.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote zitakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ufalme, utawala na ukuu wa falme zote duniani watapewa watu wa watakatifu wa Mungu Mkuu. Ufalme wao utakuwa wa kudumu milele, na tawala zote zitawatumikia na kuwatii.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, ufalme na nguvu za kutawala na ukuu wa ufalme wote ulioko chini ya mbingu utakapopewa ukoo wa watakatifu wake Alioko huko juu, ufalme wake ni wa kale na kale, nazo nguvu zote zitawalazo zitamtumikia na kumtii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ufalme, utawala na ukubwa wa falme zote katika dunia watapewa kwa watu wa watakatifu wa Mungu Mukubwa. Ufalme wao utakuwa wa kudumu milele, na tawala zote zitawatumikia na kuwatii.