Daniel 7:4 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, na alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikiwa namwangalia, mabawa yake yalingolewa, naye akainuliwa na kusimama kwa miguu miwili kama binadamu. Kisha, akapewa akili ya binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa ya tai. Nikatazama hadi mabawa yake yalipong’olewa, naye akainuliwa katika nchi, akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, na alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikiwa namwangalia, mabawa yake yaling'olewa, naye akainuliwa na kusimama kwa miguu miwili kama binadamu. Kisha, akapewa akili ya binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikatazama mpaka mabawa yake yalipong'olewa naye akainuliwa katika nchi akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikatazama mpaka mabawa yake yalipong’olewa, naye akainuliwa katika nchi, akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wa kwanza alikuwa kama simba, lakini alikuwa na mabawa ya tai, nikamtazama, mpaka mabawa yake yakinyonyolewa manyoya, akachukuliwa nchini, akasimamishwa kwa miguu miwili kama mtu, akapewa hata moyo wa kimtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyama wa kwanza alikuwa kama simba, na alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikiwa ninamwangalia, mabawa yake yaliongolewa, naye akainuliwa na kusimama kwa miguu miwili kama mutu. Kisha, akapewa akili ya kimutu.