Daniel 7:5 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnyama wa pili alikuwa kama dubu ambaye upande wake mmoja ulikuwa umeinuka. Kinywani mwake alikuwa na mbavu tatu alizozishikilia kwa meno yake. Sauti ikamwambia, ‘Haya, kula nyama nyingi kadiri uwezavyo.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, aliyefanana na dubu. Upande wake mmoja alikuwa ameinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama, ushibe!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnyama wa pili alikuwa kama dubu ambaye upande wake mmoja ulikuwa umeinuka. Kinywani mwake alikuwa na mbavu tatu alizozishikilia kwa meno yake. Sauti ikamwambia, ‘Haya, kula nyama nyingi kadiri uwezavyo.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara nikaona nyama mwingine, ndio wa pili, alifanana na nyegere, alisimama upande mmoja tu, namo kinywani mwake alishika mbavu tatu kwa meno yake, akaambiwa: Inuka, ule nyama nyingi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyama wa pili alikuwa kama dubu ambaye upande wake mumoja ulikuwa umeinuka. Na katika kinywa chake alikuwa na mifupa mitatu ya mbavu aliyoishika kwa meno yake. Sauti ikamwambia: Simama, ukule nyama nyingi kadiri unavyoweza.